1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU Kutuma ujumbe wa Haki za Binadamu Cuba

27 Mei 2023

Umoja wa Ulaya umesema utatuma ujumbe maalum wa haki za binadamu nchini Cuba baadae mwaka huu, kujadili athari za maandamano dhidi ya serikali yaliyofanyika mwezi Julai mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4Rt42
Kuba Proteste 11.07.2021, Gegendemo mit Miguel Diaz-Canel
Picha: Yander Zamora/Agencia EFE/IMAGO

Mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borrell, amesema licha ya ujumbe huo utakaoongozwa na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya wa Haki za Binadamu Eamon Gilmore utachambua hali liyojitokeza kabla, wakati na baada ya maandamano na kukamatwa kwa waandamanaji.

Soma zaidi: Marekani yakosolewa na Iran kwa kuunga mkono maandamano ya Cuba

Mamia ya Wacuba bado wangali gerezani baada ya maandamano hayo makubwa zaidi, tangu yalipofanyika mapinduzi yaliyoongozwa na kiongozi wa zamani Fidel Castro mwaka 1959 huku serikali ikisema, waliofungwa walikuwa na hatia ya kushambulia, kuharibu mali na uchochezi.