1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaFinland

Finland yaidhinisha mkataba wa ulinzi na Marekani

1 Julai 2024

Bunge la Finland limeidhinisha kwa pamoja mkataba wa ulinzi na Marekani, utakaoruhusu kuimarishwa kwa uwepo wa jeshi la Marekani na uhifadhi wa nyenzo za ulinzi nchini Finland.

https://p.dw.com/p/4hkib
Finnland NATO Militärübung Steadfast Defender
Wanajeshi wa Finland wakiendesha kifaru mpaka wa nchi hiyo na Uswidi Picha: Jonathan Nackstrand/AFP/Getty Images

Mkataba huo unalenga kuimarisha uwezo wa kiusalama na ulinzi wa Finland, baada ya nchi hiyo ya Nordic kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO mwezi Aprili 2023, kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kigeni, Kimmo Kiljunen ameitaja hatua ya kupitishwa kwa makubaliano ya hayo kama wakati wa kihistoria. 

Soma pia: Finland kuwazuia watafuta hifadhi kuingia nchini humo

Makubaliano hayo yanaipa Marekani idhini ya kufikia kambi 15 za kijeshi nchini Finland, mafunzo kutoka kwa vikosi vya Marekani, na kuweka nyenzo za ulinzi katika ardhi ya Finland.

Marekani imehitimisha makubaliano kama hayo na nchi nyingine 11 za jumuiya ya kujihami ya NATO, Sweden, Norway na Denmark.