1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Freeman Mbowe akubali kushindwa uenyekiti CHADEMA

22 Januari 2025

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimechagua Tundu Lissu kuwa kiongozi mpya kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, wakati ambapo kinakabiliwa na ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4pSQR
Tanzania Daressalam 2024 | Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema anaemaliza muda wake Freeman MbowePicha: Eric Boniface/DW

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amechaguliwa kuwa kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA,katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo akimbwaga kiongozi wa muda mrefu Freeman Mbowe. 

Lissu alipata ushindi mwembamba katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA. 

Mbowe ambaye ameiongoza CHADEMA kwa miongo miwili ampongeza Lissu ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho. 

Soma pia:Lissu ambwaga Mbowe uenyekiti CHADEMA 

Mabadiliko hayo ya uongozi yanatokea katikati ya mbinyo unaovikabili vyama vya upinzani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na misuguano ya ndani ya vyama ambayo wachambuzi wanasema inaweza kuteteresha nafasi yao kuelekea uchaguzi unaokuja. 

Tanzania itafanya uchaguzi mkuu mnamo mwezi Oktoba ambao utakuwa wa kwanza chini ya Rais Samia Suluhu aliyeingia madarakani mwezi Machi 2021 kufuatia kifo cha