1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 yalaani mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran

18 Aprili 2024

Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa saba yaliyoimarika kiviwanda duniani, G7, wamelaani mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya Israel, huku pia yakiahidi kutumia mali za Urusi zilizofungiwa kusaidia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ev6a
Iran | makombora
Makombora ya Iran yakioneshwa kwenye gwaride la Siku ya Majeshi ya Iran tarehe 17 Aprili 2024.Picha: Vahid Salemi/AP/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wao, mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za mataifa yanayounda kundi la G7 walisema wangelifanya kila wawezalo kuhakikisha uratibu wa karibu wa hatua yoyote ya baadaye ili "kupunguza uwezo wa Iran kupata, kuzalisha, au kuhamisha silaha zinazochangia katika kuyumbisha shughuli kwenye Ukanda wa Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.

Soma zaidi: Israel yahimizwa kutojibu shambulizi la Iran

Kwa upande mwengine, mawaziri hao walisema wako tayari kuisaidia Ukraine kukidhi mahitaji yake ya haraka wakati inapopambana dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Mawaziri hao walikuwa wanakutana kandoni mwa mikutano ya msimu wa machipuko ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia mjini Washington, Marekani.