1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Gabon: Jeshi lamtangaza Brice Nguema kuwa rais wa mpito

31 Agosti 2023

Viongozi wa mapinduzi nchini Gabon jana walimchagua jenerali Brice Oligui Nguema kuwa rais wa mpito baada ya kutwaa madaraka na kumkamata rais Ali Bongo.

https://p.dw.com/p/4VnU3
General Brice Oligui Nguema
Picha: Handout/Gabon 24/AFP

Rais huyo aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumamosi iliyopita, hivi sasa anashikiliwa katika kifungo cha nyumbani baada ya jeshi kuyafuta matokeo hayo na kusimamisha shughuli za taasisi zote za serikali pamoja na kufunga mipaka ya nchi.

Soma pia:Jeshi lamtangaza mkuu wa kitengo cha walinzi wa rais Brice Nguema kama kiongozi wa mpito Gabon

Jeshi limesema limemkamata mmoja wa wanawe,wa kiume  kwa tuhuma za  uhaini.

 Mapinduzi hayo yamelaaniwa na Umoja wa Afrika huku Nigeria ikitowa tahadhari juu ya kile ilichokiita kuenea kwa tawala za kimabavu,katika bara hilo ambako wanajeshi wamechukuwa madaraka katika nchi nyingine tano tangu mwaka 2020.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW