SiasaMarekani
Hafla ya kuapishwa Trump kufanyika ndani ya jengo la Bunge
18 Januari 2025Matangazo
Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika muda wa mikaa 40 kuchukuliwa kwa uamuzi kama huu wa kuhamisha tukio hili muhimu la kidemokrasia kufanyika ndani kuliko nje kama ilivyozoeleka.
Rais wa mwisho kuapishwa ndani ya jengo ilikuwa Rais Ronald Reagan mnamo mwaka 1985 alipokula kiapo kuanza muhula wake wa pili.
Hafla ya kuapishwa kwa Trump itahudhuriwa na viongozi mbalimbali. Hata hivyo Trump amesema kuwa sherehe zingine zote zitafanyika kama ilivyopangwa.