Haiti na Kenya zaanzisha uhusiano wa kidiplomasia
21 Septemba 2023Matangazo
Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na mijadala ya kimataifa kuhusu uwezekano wa Kenya kuongoza kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa kusaidia polisi wa Haiti, wenye rasilimali chache, kupambana na magenge ya uhalifu ambayo yanakadiriwa kudhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo.
Mapema wiki hii, afisa mmoja wa Marekani alisema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza ndani ya muda wa wiki moja, kupiga kura kuidhinisha kikosi cha kimataifa kwa ajili ya Haiti.
Serikali ya Port-au-Prince iliomba msaada wa kimataifa mwezi Oktoba, lakini licha ya wito wa mara kwa mara wa Umoja wa Mataifa, ombi hilo halikujibiwa hadi pale Kenya iliposema mwezi Julai kuwa ilikuwa tayari kuongoza Ujumbe kama huo.