MigogoroAfrika
Hali ya usalama yaendelea kuzorota Goma nchini Kongo
19 Februari 2024Matangazo
Baadhi ya raia wameanza kuondoka katika jiji hilo baada ya mabomu mawili kulipuka siku ya Jumamosi katika uwanja wa ndege mjini Goma na kusababisha uharibifu mkubwa.
Jeshi la Kongo limesema lilikuwa shambulio la droni liliendeshwa na jeshi la Rwanda.
Soma pia:Bomu laupiga uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa Kongo
Marekani imelaani hali ya kuongezeka kwa ghasia zinazofanywa na waasi wa M23 katika ardhi ya Kongo, huku kukiwepo harakati za kikanda za kutafutia suluhu mzozo huu kati ya DRC na Rwanda ambayo inashutumiwa kuwafadhili waasi hao wa M23 - tuhuma ambazo serikali mjini Kigali imekuwa mara kadhaa ikizikanusha.