Hamas yakubali pendekezo la Marekani juu ya mateka wa Israel
6 Julai 2024Hamas imekubali pendekezo la Marekani la kuanza mazungumzo ya kuwaachilia mateka wa Israel, wakiwemo askari na wanaume, hatua hiyo inajiri baada ya siku 16 za awamu ya kwanza ya makubaliano yenye lengo la kufikisha mwisho vita vya Gaza, hayo ni kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Hamas.
Soma zaidi. Kundi la Hamas lafahamisha Hezbollah kuwa limekubali kusitisha mapigano Gaza.
Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu limeweka sharti la kwamba ni lazima Israel iahidi kusitisha mapigano ya kudumu kabla ya wao kusaini makubaliano ambayo yangeruhusu mazungumzo ya kipindi cha wiki sita.
Upande wa timu ya mazungumzo ya Israel umeeleza kuwa hiyo ni hatua muhimu ya kufanikiwa kwa makubaliano. Hatua hiyo ni tofauti na kipindi cha miezi tisa iliyopita huko Gaza ambapo Israel ilisema masharti yaliyoambatanishwa na Hamas hayakubaliki.
Soma zaidi. Netanyahu kupeleka wawakilishi majadiliano ya kusitisha vita Gaza
Kulingana na maafisa wa afya wa Gaza mzozo huo umegharimu maisha ya zaidi ya wapalestina 38,000 tangu Israel ilipoanza kulishambulia eneo hilo baada ya shambulizi la Hamas la Oktoba 7 mwaka uliopita lilowaua watu 1200 na wengine 250 wakachukuliwa mateka.