Hezbollah yakiri Israel kumuua kamanda wake mwingine
29 Septemba 2024Mauaji hayo yametokea siku moja baada ya kundi hilo la Lebanon kukiri kuuawa kwa makamanda wake kadhaa, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Hassan Nasrallah.
Taarifa hiyo imekuja saa kadhaa baada ya shambulio la ndege la Israel, kaskazini-mashariki mwa Lebanon kuwaua watu 11. Israel imesema zaidi ya wanachama 20 wa Hezbollah waliuawa pamoja na Nasrallah.
Umoja wa Mataifa unasema idadi ya watu waliohamishwa na mzozo huo kutoka kusini mwa Lebanon imeongezeka zaidi ya maradufu na sasa inasimama kwa zaidi ya 211,000.
Wakati huo huo, vyanzo viwili vya habari vimesema shambulizi la Israel limemuua mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la Kisunni la Jama'a Islamiya Mohammad Dahrouj.
Kundi hilo limeripotiwa kufanya mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel mwaka uliopita, na Israel imefanya mashambulizi yaliowalenga viongozi wengine waandamizi wa kundi hilo.