1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

HRW na Amnesty yataka viongozi kuwaachia huru wafungwa Niger

26 Oktoba 2023

Mashirika hayo yamesema, tangu mapinduzi ya mwezi julai yaliyomuondoa madarakani Rais Mohammed Bazoum, rais huyo pamoja na mkewe na mwanawe bado wamezuiliwa katika makao ya rais.

https://p.dw.com/p/4Y48y
Rais aliyepinduliwa madarakani Mohammed Bazoum
Rais aliyepinduliwa madarakani Mohammed BazoumPicha: Sophie Garcia/AP Photo/picture alliance

Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch leo yametoa wito kwa utawala wa kijeshi nchini Niger kuwaachia huru wale wote wanaozuiliwa nchini humo na kutoa nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Katika taarifa, mashirika hayo yamesema, tangu mapinduzi ya mwezi julai yaliyomuondoa madarakani Rais Mohammed Bazoum, rais huyo pamoja na mkewe na mwanawe bado wamezuiliwa katika makao ya rais.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mawaziri kadhaa waliokuwa wakihudumu katika serikali hiyo ya Bazoum, wamefungwa jela nchini humo. Mashirika hayo yamezidi kueleza kwamba waandishi wa habari wa Niger na wa kimataifa wanatishiwa na kupitia mashambulizi ya mitandaoni na hata ya kimwili.