IAEA yalaani mashambulizi ya Ukraine kwenye kinu cha nyuklia
8 Aprili 2024Matangazo
Mkuu wa shirika hilo alisema mashambulizi hayo yanaongeza uwezekano wa kutokea kwa ajali mbaya ya atomiki.
Kwenye taarifa aliyoituma katika mtandao wa X, Rafael Mariano Grossi, alithibitisha kuwa kinu kikuu kwenye eneo hilo kilishambuliwa mara tatu, akisema hilo ni jambo lisilokubalika.
Soma zaidi: IAEA yatoa onyo dhidi ya kukifungua kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia
Hayo yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu Novemba 2022, wakati mkuu huyo waIAEA alipotangaza hatua tano za kuchukuliwa ili kuepusha uwezekano wa ajali mbaya ya mionzi ya nyuklia kwenye kinu hicho.
Maafisa kwenye kinu hicho walisema hakukuwa na madhara kwa kinu hicho wala mtu aliyeuawa wala kujeruhiwa kwa mashambulizi hayo ya jana Jumapili.