MigogoroMashariki ya Kati
ICJ yaitaka Israel kuboresha hali ya misaada ya kiutu Gaza
29 Machi 2024Matangazo
Hatua hizo ni pamoja na kufungua vivuko zaidi vya ardhini ili kuruhusu usambazaji wa chakula, maji, mafuta na vifaa vingine muhimu.
Mahakama hiyo imesema imechukua hatua za muda katika kesi iliyoanzishwa na Afrika Kusini ikiishutumu Israel kwa vitendo vya mauaji ya halaiki katika operesheni yake ya kijeshi huko Gaza baada ya mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas Oktoba 7 mwaka jana.
Soma pia: UN yaitaka Israel iondoe marufuku ya misaada Gaza
Israel imekuwa ikikanusha kufanya mauaji ya kimbari na kuishutumu Afrika Kusini kwa kujaribu kufifisha haki na wajibu wa Israel kujilinda na kutetea raia wake. Hayo yanajiri wakati mapigano yakiendelea huko Gaza na Wizara ya Afya imesema hadi sasa watu 32,552 wameuawa katika mzozo huo.