1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

Idadi ya waliokufa kwa mafuriko Rwanda yafikia 130

4 Mei 2023

Mafuriko na maporomoko ya udongo kutokana na mvua kubwa, yamesababisha vifo vya watu 130 nchini Rwanda wiki hii.

https://p.dw.com/p/4QuXl
Maafa ya mafuriko nchini Rwanda
Mbali ya vifo, mafuriko yaliyotokea Rwanda yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali.Picha: JEAN BIZIMANA/REUTERS

Naibu msemaji wa serikali Alain Mukuralinda amesema hayo na kuongeza kuwa zaidi ya nyumba 5,000 zimeharibiwa.

Kulingana na Mukuralinda, barabara, madaraja, hospitali moja na vituo vingine vitano vya afya ni kati ya miundombinu iliyoharibiwa.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Rwanda imetahadharisha kwamba mvua nyingi bado zinatarajiwa.

Baadhi ya nchi za kanda ya Afrika Mashariki ikiwemo kusini magharibi mwa Uganda, pia zinakumbwa na mvua kubwa.

Nchini Uganda, mwandishi mmoja wa habari Simone Schlindwein ameliambia shirika hili la habari kwamba vijiji kadhaa vilisombwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa ya hivi karibuni katika kanda hiyo.