1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF na Uganda zakubaliana kuhusu mkopo

Josephat Charo
3 Juni 2021

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limefikia makubaliano na Uganda kuhusu mpango wa thamani ya dola bilioni moja chini ya mkopo utakaorefushwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

https://p.dw.com/p/3uNtP
USA Weltbank-Zentrale in Washington
Picha: Reuters/Y. Gripas

Hayo yamesemwa na shiriki la IMF siku ya Jumatanoa. Amine Mati, Mkuu wa timu ya IMF iliyofuatilia hali nchini Uganda kwa njia ya mtandao mapema mwaka huu, amesema mpango unaofadhiliwa na IMF nchini humo unasaidia hatua inayofuata ya utekelezaji wa mikakati ya kupambana na COVID-19 na kuimarisha misingi ya ukuaji uchumi jumuishi unaoongozwa na sekta binafsi.

Soma pia: Uganda kuwaomba wakopeshaji kuchelewesha ulipaji madeni

Makubaliano hayo yanasubiri kuridhiwa na uongozi wa IMF. Mwezi uliopita Uganda ilisema ilikuwa imeomba mkopo kutoka kwa IMF ili kuimarisha hazina yake ya fedha baada ya janga la COVID-19 kuuathiri uchumi wake.

Mwaka uliopita IMF iliipa Uganda mkopo wa dola milioni 400.