SiasaAsia
Imran Khan afutiwa mashitaka ya mauaji
28 Agosti 2023Matangazo
"Mungu Mkubwa" aliandika wakili wa Khan, Naeem Panjutha, kwenye ukurasa wa X, akiongeza kuwa mahakama imeondoa madai yaliyohusiana na mauaji ya mwanasheria mmoja katika mji wa Quetta kusini mwa nchi hiyo.
Soma zaidi: Kiongozi wa upinzani akamatwa Pakistan kwa kosa la kufichua siri za serikali
Khan aliyefunguliwa madai ya mauaji mwezi Juni, anakabiliwa na kesi zaidi ya 100, tangu alipoondolewa madarakani katika kura ya bunge ya mwezi Aprili ya kutokuwa na imani naye, baada ya mvutano kati yake na jeshi lenye nguvu kubwa la Pakistan.
Mahakama kuu mjini Islamabad pia inatazamiwa kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na Khan akitaka kusimamishwa madai ya ufisadi dhidi yake hati.