Iran na Syria zalaani mashambulizi ya Marekani nchini Syria
26 Machi 2023Mashambulizi hayo yalikuwa dhidi ya vikosi vyenye uhusiano na Iran, na yalisababisha vifo vya watu 19.
Jeshi la Marekani lashambulia nchini Syria na kuua watu 10
Washington inasema ilitekeleza mashambulizi hayo baada ya shambilio la ndege zisizo na rubani za Iran kusababisha kifo cha mkandarasi wa Marekani nchini Syria.
Wizara ya mambo ya nje ya Syria imelaani mashambulizi ya Marekani katika eneo lake, ikisema Washington imedanganya kuhusu kile kilicholengwa katika mashambulizi hayo na kwamba imevunja ahadi yake ya kusitisha vitendo vya kuyadhibiti maeneo yake.
Marekani ina takriban wanajeshi 900 katika vituo vyake kaskazini mashariki mwa Syria wanaoendelea kupambana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS na kuunga mkono Kikosi cha Kidemokrasia cha Syria kinachoongozwa na Wakurdi, ambacho kinadhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.