1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ofisi za umma kufungwa Iran kufuatia wimbi la joto kali

27 Julai 2024

Mamlaka nchini Iran zimeamuru kupunguza masaa ya kazi siku ya Jumamosi na kufungwa kwa ofisi za serikali na maduka siku ya Jumapili kufuatia wimbi la joto kali.

https://p.dw.com/p/4ipDn
Vijana wa Iran wakitembea mjini Tehran
Vijana wa Iran wakitembea mjini TehranPicha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Mji mkuu Tehran umerekodi hadi nyuzijoto 42 katika kipimo cha Celsius. Shirika la habari la la serikali IRNA limeeleza kuwa benki, ofisi za umma na taasisi zote nchini Iran zitafungwa siku ya Jumapili ili kulinda afya ya watu na kuhifadhi nishati kutokana na joto kali na kusisitiza kwamba ni huduma za dharura pekee na mashirika ya matibabu ndiyo yataruhusiwa kufanya kazi.

Soma pia: Joto lalazimisha Iran kuzifunga ofisi muhimu

Vyanzo vilivyo karibu na Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, vimeripoti kuwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, joto nchini Iran limekuwa likiongezeka kwa kasi ukilinganisha na maeneo mengine duniani. Mwaka jana, Iran iliamuru likizo ya siku mbili kote nchini humo kutokana na wimbi la joto kali.