Janga
Israel imefanya mashambulio makubwa Lebanon
3 Desemba 2024Matangazo
Mashambulio hayo yamefanywa na Israel kama onyo kwa kile ilichosema ni kukiukwa makubaliano ya kusitisha vita.
Kundi la Hezbollah lilifyetuwa makombora mawili kuelekea eneo la Shebaa linaloshikiliwa na Israel ambalo liko kwenye mpaka kati ya Lebanon, Syria na Israel.
Wizara ya afya ya Lebanon imesema mashambulio hayo ya pande zote mbili yanatishia makubaliano yaliyofikiwa.
Israel yasema wakazi wa Lebanon wamepigwa marufuku kurejea katika vijiji kadhaa vya eneo la kusini
Wakati huohuo wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na chama cha rais Mahmoud Abbas cha Fatah, wamekubaliana kuunda kamati ya pamoja ya kusimamia Gaza baada ya vita. Makubaliano hayo yatakayopaswa kwanza kuidhinisha na rais Abaas yametangazwa leo na wasuluhishi.