1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yaendelea kuishambulia Gaza baada kifo cha Sinwar

18 Oktoba 2024

Israel imesema imefanya mashambulizi kwenye ukanda wa Gaza Ijumaa (18.10.2024), siku moja baada ya kutangaza kumuua kiongozi wa kundi la Hamas, Yahya Sinwar.

https://p.dw.com/p/4lwZ1
Wazima moto wa Kipalestina wakijaribu kuzima moto uliosababishwa na shambulio la Israel lililopiga huko Deir al Balah, Ukanda wa Gaza
Wazima moto wa Kipalestina wakijaribu kuzima moto uliosababishwa na shambulio la Israel lililopiga huko Deir al Balah, Ukanda wa GazaPicha: Abdel Kareem Hana/AP/picture alliance /

Kwa mujibu wa idara ya ulinzi ya Gaza, waokoaji wameipata miili mitatu ya watoto kutoka kwenye vifusi vya nyumba yao kaskazini mwa Ukanda huo baada ya nyumba hiyo kushambuliwa alfajiri ya leo.

Jeshi la Israel limedai kuwa linaendeleza operesheni zake kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia, ambako hapo jana liliwauwa watu 14, kwa mujibu wa hospitali mbili za eneo hilo.

Hayo yakijiri, tathmini iliyofanywa na Umoja wa Mataifa inasema kiasi cha wakaazi 345,000 wa Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na janga kubwa la njaa kwenye majira haya ya baridi.

Kutokana na idadi kubwa ya raia waliouawa kwenye mashambulizi yake, Israel inakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa jinsi inavyoviendesha vita hivi, ukiwemo ukosoaji wa mshirika na mfadhili wake mkuu, Marekani.