Mashambulizi ya Israel yauwa dazeni kadhaa Gaza
8 Januari 2025Madaktari wamesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya Sheikh Radwan, Zeitoun, na Deir Al Balah katikati mwa Gaza. Miongoni mwa waathirika ni watoto, huku familia moja ikieleza huzuni yao baada ya kupoteza mpendwa wao.
Mayson Abu Al Qomsan, ambaye alimpoteza mtoto wa dada yake katika shambulio hilo, amesema: "Dada yangu alikuwa kwenye hema na walimrushia kombora yeye na watoto wake. Kosa lao lilikuwa nini? Naapa hawakuwa na uhusiano na chochote. Walikuwa wanapigwa na baridi, sasa wameuawa na mashambulizi ya Israel. Hili, kwa Mungu, ni dhambi."
Soma pia: Vyanzo: Mashambulizi ya Israel yawaua zaidi ya watu 20 Gaza
Huku mashambulizi yakizidi, juhudi za upatanishi zimeongezwa kasi. Chanzo karibu na mazungumzo hayo kimedokeza kuwa kikao cha hivi karibuni kimeweka mkazo mkubwa ikilinganishwa na vikao vya awali. Marekani inaendelea kushinikiza pande zote kufikia makubaliano ya kusitisha vita ili kumaliza mgogoro huu wa muda mrefu.