Japan yakumbwa na mvua kubwa na maporomoko ya ardhi
10 Julai 2023Matangazo
Mtu mmoja amefariki na maelfu ya wengine wameyahama makazi yao kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika kisiwa cha Kyushu kusini magharibi mwa Japan. Huduma ya treni ya mwendo kasi imesitishwa kati ya Hiroshima na Fukuoka.
Aliyefariki ni mwanamke mwenye umri wa miaka 70 baada ya nyumba yake kusombwa na maporomoko ya ardhi katika mkoa wa Fukuoka. Shirika la habari la Japan NHK limefahamisha kuwa katika mkoa wa Saga, watu wawili hadi sasa hawajulikani waliko.
Soma kuhusu: Mataifa kadhaa ya Asia yakumbwa na mvua kubwa
Mkurugenzi wa kitengo cha utabiri wa Hali ya Hewa huko Japan, Satoshi Sugimoto amesema mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kaskazini mwa kisiwa cha Kyushu hadi kesho Jumanne, na onyo limetolewa kwa wilaya za Fukuoka na Oita.