Jenerali Nguema aapishwa kuwa rais wa mpito Gabon
4 Septemba 2023Ameahidi kurudisha utawala wa kira kupitia uchaguzi huru utakaozingatia uwazi na wenye kuaminika.
Katika hotuba yake baada ya kula kiapo hii leo,jenerali Nguema amesema uchaguzi utakaoandaliwa nchini humo utakuwa ndio msingi wakuyakabidhi madaraka kwa serikali ya kiara.
Hata hivyo hakutowa muda kuhusu ratiba ya kufanyika mchakato huo.
Soma pia:Gabon yafungua mipaka siku tatu baada ya mapinduzi
Kadhalika amewataka Wagabon kushiriki katika mchakato wa kuandika katiba mpya itakayoidhinishwa kupitia kura ya maoni.
"Katiba ndio msingi wa taifa. Inalinda taasisi zake na kanuni zake."
Amesema mifumo ya uwakilishwaji haikuwa tena na uwezo wa kuhakikisha usalama wa raia.
"Ni muhimu kwa watu wa Gabon wa matabaka yote ya maisha kukubaliana kuiidhinishia katiba mpya kupitia kura ya maoni''
Jenerali Oligui mwenye umri wa miaka 48 amesema ameshangazwa na ukosoaji unaotolewa na nchi za kigeni juu ya mapinduzi yaliyoufikisha mwisho utawala wa muda mrefu wa kifamilia wa rais Ali Bongo Ondimba na babayake Omar Bongo aliyefariki mwaka 2009.