1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Marekani kurejea tena Chad kwa mazungumzo

2 Mei 2024

Jeshi la Marekani linapanga kurejea Chad kwa mazungumzo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja yenye lengo la kufanya maboresho ya makubaliano ambayo yatatoa nafasi ya askari wake kuweka kambi katika ardhi ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4fP9Q
USA Washington | General Michael Langley
Kamanda Michael Langley akizungumza wakati wa kikao cha Seneti cha Huduma za Kivita, Julai 21, 2022, mjini Washington.Picha: Mariam Zuhaib/AP/picture alliance

Hayo yamesema na Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Marekani kwa Afrika Jenerali Michael Langley, katika mkutano wa kilele wa pili wa Vikosi vya Wanamaji wa Afrika, au AMFS uliofanyika mjini Accra, Ghana.

Amesema kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Chad kulitarajiwa kuwa ni kwa muda mfupi tu, na Chad ilikuwa imewasiliana na Washington kwamba ilitaka kuendeleza ushirikiano wa kiusalama baada ya uchaguzi wa rais.

Mwezi uliopita Marekani ilisema inaondoa idadi kubwa ya wanajeshi wake takriban 100 kutoka Chad baada ya serikali kuhoji uhalali wa shughuli zao huko.