1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uganda limemuuwa kamanda wa kundi la waasi DRC

26 Agosti 2023

Jeshi la Uganda limemuuwa mmoja wa makamanda wa kundi la waasi wa ADF lenye mafungamano na wanamgambo wa dola la Kiislamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4VbaG
Uganda | Soldaten der UPDF an der Grenze zu Kongo
Picha: Glody Murhabazi/AFP/Getty Images

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana Ijumaa imesema, kamanda huyo aliyetambulika kwa jina moja la Fazul, alikuwa raia wa Tanzania na amekuwa akiendesha operesheni katika bonde la Mwalika kwenye mkoa wa Kivu. 

Waasi wa ADF watanua harakati zao Congo

Waasi wa ADF wamekuwa wakiendesha shughuli zao kwenye misitu Mashariki mwa Kongo kwa zaidi ya miongo miwili na wamekuwa wakifanya mashambulizi ndani ya nchi hiyo na wakati mwingine nchini Uganda.

Kundi hilo halikutoa taarifa yoyote ya haraka kuhusu kifo cha kamanda huyo. Kampala kwa kushirikiana na jeshi la Congo imekuwa ikipambana na makundi ya wabeba silaha kwa karibu miaka miwili sasa.