1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la ADF latanua operesheni zake Congo

21 Juni 2023

Kundi la Uganda la Allied Democratic Forces ADF linatanua harakati zake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia ufadhili wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu. Hayo yamesemwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4SsS4
Kongo I Soldaten während einer gemeinsamen Militäroperation gegen bewaffnete Kräfte in Beni
Picha: Alain Uaykani/Xinhua News Agency/picture alliance

Kundi la ADFlilianzisha uasi nchini Uganda lakini limekuwa likiendesha shughuli zake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990. Limetangaza utiifu kwa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS mnamo 2019. Kundi hilo liliwaua watu wapatao 37 katika shambulizi kwenye shule moja ya sekondari magharibi mwa Uganda karibu na mpaka wa Congo Ijumaa usiku wiki iliyopita.

Soma zaidi: Maswali yazuka kuhusu shambulizi kali la shule la ADF

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema katika ripoti yao kwamba licha ya operesheni ya pamoja dhidi ya kundi la ADF iliyofanywa na serikali ya Congo na majeshi ya Uganda, iliyopewa jina Operation Shujaa, kundi hilo limewatuma wapiganaji wake kupanga mashambulizi kilometa nyingi mbali kabisa na eneo lake la kawaida la kuendesha harakati zake mashariki mwa Congo.

Ripoti inasema katika mkoa wa Kivu Kaskazini Operation Shujaa ilikuwa na mafanikio dhidi ya kundi la ADF ambalo liko chini ya vikwazo. Hata hivyo kundi hilo limefuatulia kutanua himaya yake nje ya mikoa ya Kivu kaskazini na Ituri na kuendelea kufanya mashambulizi ya mauaji dhidi ya raia. Ripoti imeendelea kueleza kuwa ADF imeongeza harakati zake katika mkoa wa Kivu Kusini katika miezi ya hivi karibuni na imetafuta kuwasajili wapiganaji wapya na kufanya mashambulizi katika mji mkuu Kinshasa na katika mkoa wa Haut-Uele.

Demokratische Republik Kongo | Soldaten von Uganda und DRC | Archivbild
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Operation Shujaa yaendelea

Msemaji wa serikali ya Congo Patrick Muyaya aliuambia mkutano wa waandishi habari Jumatatu wiki hii kwamba inafaa kutambua kuwa lengo la ADF ni kufanya vitendo vya kigaidi vinavyoibua hamasa kubwa na kuzungumziwa katika vichwa vya habari ili kujitangaza. Muyaya aidha alisema jeshi linapiga hatua dhidi ya ADF kupitia operesheni yake ya pamoja na Uganda, hususan katika ngome za kundi hilo ambako wameharibu vituo vya kutoa mafunzo na maeneo mengine.

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa pia limeripoti kuhusu taarifa mpya ya vyanzo vya fedha kwa kundi la ADF wakisema wameorodhesha msaada wa fedha kutoka kwa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS na mafungamano kati ya ADF na vikundi vya Dola la Kiislamu nchini Afrika Kusini.

Ripoti imesema Daesh, jina la kiarabu la kundi la Dola la Kiislamu, imetoa msaada wa fedha kwa ADF tangu 2019, kupitia mpango wa fedha ambao ni vigumu kutambulika, unaoanzia nchini Somalia na kwenda mpaka Afrika Kusini, Kenya na Uganda.

Watalaamu wa Umoja wa Mataifa pia walipata ushahidi wa mafungamano na ushirikiano wa kimuundo kati ya kundi la ADF na kundi la wanamgambo wa Ahlu Sunnah Wal Jama'a (ASWJ) nchini Msumbiji, ambalo pia limetangaza utiifu kwa kundi la Dola la Kiislamu.

(rtre)