1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Jimmy Carter atakumbukwa kwa lipi barani Afrika?

9 Januari 2025

Jimmy Carter aliyefariki akiwa na umri wa miaka 100, alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kufanya ziara ya kiserikali katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4oyAq
Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter (kulia) akisalimiana na Nelson Mandela
Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter (kulia) akisalimiana na Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson MandelaPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Jimmy Carter aliwahi kusema kuwa miongoni mwa mafanikio yake makubwa ilikuwa kuisaidia Zimbabwe kwenye mpito wake wa kuelekea uhuru kutoka kwenye utawala kandamizi wa wazungu. Zimbabwe ilipopata uhuru mnamo mwaka 1980, Carter aliipongeza hatua hiyo na kumkaribisha Waziri Mkuu mpya na ambaye baadaye alikuja kuwa rais Robert Mugabe katika Ikulu ya White House huku akinukuu kauli ya Martin Luther King Jr kwamba "Udhalimu popote pale ni tishio kwa haki kila mahali."

Afrika, yenye idadi ya watu zaidi ya bilioni moja na inayotarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwaka 2050, ndipo urathi wa unakodhihirika zaidi. Kabla ya urais wake, viongozi wa Marekani walionekana kuipa kisogo Afrika, licha ya kushuhudia vuguvugu za kupigania uhuru mnamo miaka ya 1960 na 1970.

Soma pia: Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter afariki dunia

Rais Jimmy Carter alijaribu kuiondoa nadharia iliyokuwa imeenea kwamba Marekani imelitupilia bara la Afrika. Alipoitembelea Nigeria mwaka 1978, nchi yenye watu wengi zaidi barani humo, Carter alisema kuwa zama za watu kuiona Marekani kuwa taifa katili zimekwisha na kuwa ulikuwa wakati wa kuanzisha mahusiano mapya. Ili kuonyesha mahusiano ya kirafiki, Carter alimtania rais wa Nigeria wa wakati huo Olesegun Obasanjo kwamba wangelianza pamoja kilimo cha karanga.

Jeneza la aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter
Jeneza la aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy CarterPicha: J. Scott Applewhite/AP Photo/picture alliance

Wakati dunia ikiendelea kuomboleza kifo chake, Wamarekani wamemuaga aliyekuwa rais wao Jimmy Carter, aliyefariki dunia tarehe 29 Desemba, 2024 akiwa na umri wa miaka 100. Mazishi rasmi ya kitaifa yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi jijini Washington. Taasisi yake imeendelea na kazi katika vijiji vya Afrika ikilenga kutimiza azma yake ya kuutokomeza ugonjwa wa ndui ambao umekuwa ukiwatesa mamilioni ya watu.

Carter: "Kwa muda mrefu nchi yetu iliipuuza Afrika"

Katika mwaka wake wa kwanza wa uongozi, Carter aliiambia kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic kwamba kwa muda mrefu sana, Marekani haikulitilia maanani bara la Afrika. Baadaye viongozi wa Afrika walianza kupokea mialiko kwenye Ikulu ya Marekani na walikuwa na shauku ya kufahamu ni kwa faida gani walialikwa na taifa lenye nguvu zaidi ulimwenguni.

Mvutano wa Vita Baridi ulipelekea  Jimmy Carter kuliekea bara la Afrika wakati Marekani na Umoja wa Kisovieti zilikuwa zikishindana kukuza ushawishi wao. Lakini Carter alitumia uzoefu wake wa mapokeo ya kimisionari pamoja na masaibu ya ubaguzi wa rangi na ukosefu wa haki aliyoyashuhudia kusini mwa Marekani alikozaliwa.

Rais Carter alifahamu namna ya kutumia kauli njema kwa viongozi wa Afrika. Alipotembelewa na rais wa Zambia Kenneth Kaunda alisema kuwa eneo hilo ghafla kuliwa na hali ya hewa safi ambayo inatia nguvu.

Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter akiwa na mkewe Rosalynn Carter
Aliyekuwa rais wa Marekani Jimmy Carter akiwa na mkewe Rosalynn CarterPicha: Olivier Douliery/dpa/picture alliance

Baada ya safari yake ya kwanza barani Afrika, Carter alisema kuwa viongozi karibu wote wa Afrika walikuwa na mtazamo mmoja wa kwamba wanataka kusimamia mambo yao wenyewe, kuwa na mahusiano na mataifa Umoja wa Kisovieti, Marekani na mataifa ya Ulaya Ulaya bila ya kuchagua upande mmoja. Msimamo ambao unaakisi hali halisi ya sasa ambapo mataifa ya China, Urusi na Marekani yanapambana kukuza ushawishi wao na kujipatia malighafi za bara la Afrika.

Soma pia: Viongozi wa ulimwengu wamuenzi Jimmy Carter

Lakini imekuwa nadra kumpata mjumbe kama Carter, ambaye aliyapa kipaumbele masuala ya haki za binadamu, afya, haki za kijamii na kiuchumi pamoja na haki za kiraia na kisiasa. Alifanya safari zaidi ya 40 barani Afrika baada ya urais wake, akikuza miradi ya maendeleo iliyolenga kuwawezesha Waafrika kuamua mustakabali wao wenyewe.

Licha ya hayo Carter aliikosoa serikali ya rais Robert Mugabe baada ya ukandamizaji uliosababisha vifo na ndipo mwaka 1980 kuongoza mgomo wa wanadiplomasia. Miaka mingi baada ya kuachia wadhifa wa Urais, Carter alizuiliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2008 kuingia Zimbabwe akikosoa hatua hiyo na kusema nchi hiyo ni aibu kwa ukanda huo. Aliikosoa pia serikali ya Afrika Kusini kutokana na vitendo vyake vya ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi (Apartheid).

Taasisi ya Jimmy na mkewe  Rosalynn Carter  iliyoanzishwa mwaka 1982 ina  jukumu la kufuatilia chaguzi za Afrika na kusimamia usuluhishi wa kusitisha mapigano kati ya vikosi vinavyopigana, lakini pia kupambana na umasikini na maradhi mbalimbali.

(Chanzo: APE)