1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Jinsi historia ya ukoloni Ufaransa yachangia ghasia za sasa?

3 Julai 2023

Vurugu nchini Ufaransa zinaonekana kupungua, lakini kitakachosalia ni dhaghabu. Suala la ubaguzi wa rangi ambalo linahusishwa na ukoloni wa zamani wa nchi hiyo mara nyingi hupuuzwa.

https://p.dw.com/p/4TMpx
Frankreich | Protest für getöteten 17-Jährigen
Picha: Eliot Blondet/picture alliance/abaca

Makabiliano kati ya polisi wa Ufaransa na waandamanaji ambao wengi ni vijana, yameibua maswali kuhusu kiwango cha machafuko hayo na uharibifu wa mali.

Lakini mada nyingine pia imeibuka. Nalo ni swali kuhusu kuuawa kwa Nahel kisha ghadhabu zilizofuata na kushuhudiwa mitaani, zinazohusishwa na ubaguzi wa rangi wa kimfumo ndani ya Ufaransa pamoja na historia ndefu ya kikoloni ya nchi hiyo.

Ufaransa imeshuhudia maandamano ya vurugu kote katika miji yake kufuatia kuuawa kwa kijana mwenye umri wa miaka 17 Nahel, mwenye mizizi ya Afrika kaskazini, aliyepigwa risasi na polisi Jumanne wiki iliyopita.

Soma pia: Utulivu unarejea nchini Ufaransa baada ya machafuko

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyaita mauaji ya Nahel kuwa ‘yasiyosameheka na hayaelezeki'. Lakini Crystal Fleming, profesa wa Sosholojia katika chuo kikuu cha Stony Brook mjini New York anatofautiana na Macron. Ameliambia shirika hili la habari la DW kwamba mauaji hayo sio fumbo bali ni ubaguzi wa rangi.

Uchunguzi wa ndani Ufaransa umebaini kuwa vijana wenye asili ya Afrika au Uarabu wako katika hatari mara 20 ya kusimamishwa na polisi mitaani kuliko wengine.
Uchunguzi wa ndani Ufaransa umebaini kuwa vijana wenye asili ya Afrika au Uarabu wako katika hatari mara 20 ya kusimamishwa na polisi mitaani kuliko wengine.Picha: Clement Mahoudeau/AFP

Ukanushaji wa Ufaransa kuhusu matendo yake

Fleming ameongeza kuwa maandamano na vurugu zilizofuata kifo cha Nahel, zinaibua maswali kuhusu ubaguzi wa rangi wa Ufaransa unaohusishwa na enzi za ukoloni. Hata wakati huo maafisa wa Ufaransa na wanasiasa walikanusha na kufuta visa hivyo, licha ya karne nyingi za ukandamizaji kwa msingi wa ubaguzi wa rangi kwa watu wake walio wachache na jamii za yaliyokuwa makoloni yake.

Ni kweli kwamba Ufaransa ilikuwa moja ya mataifa makubwa ya kikoloni. Tangu karne ya 16 hadi miaka ya 1970, kama tum engine katika bara Ulaya, waliamini "ujumbe wao wa ustaarabu ulihalalisha kunyonya kwa nguvu nchi nyingine kote ulimwenguni.

Soma pia: Ghasia zimepungua Ufaransa

Japo mapinduzi ya Ufaransa yam waka 1789 yalileta uhuru na usawa kwa wanaume wote wa Kifaransa nchini mwao, wale waliokuwa katika makoloni yao waliendelea tu kutamani haki hizo. Maisha yao ya kila siku yalitawaliwa na ukandamizaji. Waume na wanawake walilazimishwa "kuiga” utamaduni na lugha ya Kifaransa.

Maandamano ya vurugu katika mji wa Nanterre, Ufaransa
Maandamano ya vurugu katika mji wa Nanterre UfaransaPicha: Christophe Ena/AP/dpa

Historia tete ya Algeria na Ufaransa

Haswa matendo ya Ufaransa nchini Algeria yamesalia kuwa mada nyeti. Taifa hilo la kaskazini mwa Afrika lilitawaliwa mara ya kwanza mwaka 1830. Baadaye iliunganishwa katika taifa la Ufaransa. Waalgeria walipotaka uhuru wao, vita vikali vilivyosababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu hasa Waalgeria vilizuka. Vita hivyo vilisababisha mwisho wa utawala wa Ufaransa nchini humo mnamo mwaka 1962.

Kipindi saw ana hicho, Ufaransa ililazimishwa kuachilia mengi ya yaliyokuwa makoloni yake. Lakini iliendelea kushawishi uchumi na siasa za nchi hizo hususan barani Afrika.

Ghasia zaendelea Ufaransa, zaidi ya watu 1,300 wakamatwa

Zaidi ya rais yeyote aliyemtangulia, rais wa sasa wa Ufaransa Emmanuel Macron amekiri mara nyingi zaidi ‘historia ya uhalifu'  ya nchi yake wakati wa ukoloni. Ameahidi kurudisha mali zilizoibwa na pia kuanzisha tume zitakazochunguza vitendo vya Ufaransa nchini Algeria na pia katika mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Yves Herman/AP/picture alliance

Fleming: Hatua za Macron hazitoshi

Lakini wakosoaji kama Crystal Flemming, anahoji kuwa hatua hizo hazitoshi. Mnamo Januari 2023, Macron kwa mfano alisema hakukusudia kuomba msamaha kuhusu matendo ya nchi yake nchini Algeria, kwani hiyo ingevunja ushirikiano.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la haki za binadamu la Ufaransa, vijana wanaokisiwa kuwa weusi au Waarabu wapo katika hatari mara 20 zaidi ya kusimamishwa na polisi wa Ufaransa kuulizwa maswali au kupekuliwa. Mizizi ya w engi wa vijana hao ni makoloni ya zamani ya Ufaransa na wanaishi katika viunga vya miji mikubwa kama Paris, Marseille au Lyon.

Mwandishi: Marina Strauß

Tafsiri: John Juma