1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Asia Pasifiki na NATO wajiimarisha kupambana na vitisho

12 Julai 2024

Mataifa manne ya Kanda ya Asia Pasifiki siku ya Alhamisi yalilaani vikali "ushirikiano haramu wa kijeshi" kati ya Urusi na Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4iCC8
Mfumo wa makombora wa Patriot
Mfumo wa makombora wa Patriot ukifyatua kombora wakati wa luteka za kijeshi kati ya Ufilipino na Marekani, Aprili 25, 2023. Picha: Daniel Ceng Shou-Yi/ZUMA/picture alliance

Hatua hiyo ya mataifa hayo manne yaliyohudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami ya NATO mjini Washington, imeashiria namna NATO na washirika wake wanavyozidi kuimarisha uhusiano wa kupambana na kile wanachokiona kama kitisho cha pamoja cha kiusalama.

Japan, Korea Kusini, New Zealand na Australia ambayo si wanachama wa NATO wamehudhuria mkutano huo kwa mara ya tatu mfululizo.

Ikulu ya White House ya Marekani iliyakaribisha mataifa hayo ya India Pasifiki katika ushirikiano wa kuhakikisha usalama wao.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akisema watahakikisha wanashughulikia kwa pamoja changamoto za kiusalama ambazo ni pamoja na vita vya Urusi nchini Ukraine na msaada wa China nchini Urusi.