1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Olaf Scholz kuanza ziara ya siku tatu nchini China

13 Aprili 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani anaelekea China leo Jumamosi kwa ziara ya siku tatu ambayo inajumuisha mkutano na Rais Xi Jinping na kuizuru miji mingine miwili ya Chongqing na Shanghai.

https://p.dw.com/p/4eigL
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Anatarajiwa mjini Beijing mnamo siku ya Jumanne kwa mazungumzo ya ngazi ya juu ya kisiasa yatakayotuama juu ya masuala kadhaa vikiwemo vita vya Urusi na Ukraine, mivutano kuhusu hadhi ya kisiwa cha Taiwan na biashara.

Scholz ambaye anafuatana na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara na wakuu wa kampuni za Kijerumani, anatarajiwa kulizusha suala la umuhimu wa kuwepo usawa katika kulifikia soko la China, jambo ambalo makampuni ya Kijerumani yamelililamikia kwa muda mrefu.

Ana matumaini ya kuvutia mahusiano ya karibu na Beijing katika wakati Marekani na Umoja wa Ulaya zinatishia kuziwekea vigingi bidhaa kutoka China.