1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani ameapa kutetea biashara huria Ulaya

21 Januari 2025

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameapa kutetea biashara huria kama msingi wa mafanikio barani Ulaya. Scholz ameyasema hayo katika mkutano wa jukwaa la kiuchumi la kimataifa katika mji wa kitalii wa Davos.

https://p.dw.com/p/4pROv
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa Ujerumani ameyasema hayo katika mkutano wa jukwaa la kiuchumi la kimataifa katika mji wa kitalii wa Davos,uliofunguliwa siku moja baada ya rais Donald Trump kuingia madarakani na kuahidi kuweka ushuru na kodi kwa washirika wa kibiashara wa nchi yake.

Scholz pia amezungumzia kwa tahadhari matumaini yake kuhusu mahusiano kati ya Ujerumani na Marekani chini ya Trump.

Kansela Scholz wa Ujerumani asisitiza ushiriano imara na thabiti na Marekani chini ya utawala wa Trump

Ametaja kuhusu kufanyika mazungumzo mazuri na uongozi huo mpya wa Marekani akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Ulaya na Marekani ni jambo muhimu katika kuleta amani na usalama duniani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW