Scholz asisitiza ushirika na Marekani chini ya utawala mpya
20 Januari 2025Matangazo
Rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuapishiwa leo Jumatatu.
Katika maelezo yaliyochapishwa na gazeti la Rheinische Post leo Jumatatu, Scholz amesema uhusiano wa mataifa hayo unabaki kuwa muhimu kwa Ujerumani na kwa mataifa ya Ulaya.
Amesema, Marekani ilichangia pakubwa katika maendeleo ya kidemokrasia Ujerumani Magharibi.
Alipogusia suala la ulinzi wa Ulaya, Scholz amesema Marekani ndio mdhamini mkuu wa NATO na kwamba ni lazima kuwepo na uhusiano thabiti kati yao lakini akizitolea mwito pia nchi za Ulaya kuwa na uwezo wa kujifanyia maamuzi zenyewe.
Scholz amesema pia kwamba alizungumza kwa njia ya simu na Trump na kuyataja mazungumzo hayo kwamba yalikuwa muhimu na yenye tija.