1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu raia 15 wauawa Beni, DRC

14 Aprili 2024

Karibu raia 15 wameuawa katika mashambulizi ya mwishoni mwa wiki hii katika mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4ek3s
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Pichani ni wanajeshi wakiwa kwenye operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya wanamgambo katika eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 11, 2021.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Mashambulizi hayo mapya yanadaiwa kufanywa na waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, zimesema duru kwenye eneo hilo hii leo.

Kiongozi wa shirika moja la kiraia mjini humo Pepin Kavota amesema serikali inatakiwa kuchukua hatua za dharura za kuumaliza unyama huo. Amesema wengi wa waliouawa walikatwa vichwa.

Afisa mmoja katika mji wa Mulekera kaskazini magharibi mwa Beni Antoine Kambale ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa mwezi mmoja sasa eneo hilo jirani limekuwa likishambulia mara kwa mara na waasi wa ADF.

Amesema raia 14 waliuawa siku ya Ijumaa katika baadhi ya maeneo na shambulizi jipya liliwalenga wengine usiku wa kuamkia Jumapili na kuwaua watu wawili