Kenya yatuma wanajeshi zaidi nchini Haiti
19 Januari 2025Kulingana na waziri wa mambo ya ndani, Kipchumba Murkomen, maafisa hao waliondoka Kenya siku ya Ijumaa. Murkomen ameongeza kuwa misheni hiyo inayoongozwa na Kenya imepiga hatua kubwa katika kupunguza vurugu za magenge, na kupata sifa kote ulimwenguni, na kwamba ahadi ya kujitolea kwa taifa hilo la Afrika Mashariki haiyumbishwi.
Kenya ilituma wanajeshi wake Haiti kwa mara ya kwanza mwezi Juni na kufikia sasa imetuma zaidi ya wanajeshi 600. Rais William Ruto aliahidi kupeleka wanajeshi 1,000 kama sehemu ya kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Haiti.
Soma pia: Magenge ya Haiti yaendeleza ghasia nje ya mji mkuu
Vurugu za magenge zimeacha zaidi ya Wahaiti 700,000 bila makao huku wengi wakisongamana katika makazi ya muda na yasiyo safi
baada ya nyumba zao kubomolewa. Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 5,600 waliripotiwa kuuawa kote Haitimwaka jana.