Kikosi cha jeshi chashambuliwa Burkina Faso
28 Novemba 2023Vyanzo vya usalama vimeliambia shirika la habari la AFP kuwa, wanajeshi kadhaa wameuawa katika shambulio hilo bila ya kutoa idadi.
Kikosi hicho cha jeshi kinachohudumu katika ukanda wa Sahel, kilikuwa shabaha ya "shambulio kubwa la wapiganaji wa jihadi na makundi mengine ya silaha." Chanzo hicho cha usalama kimeeleza kuwa, jeshi hilo lilijibu na kuwasababishia hasara kubwa washambuliaji.
Soma pia:Jeshi la Burkina Faso laangamiza wanamgambo kaskazini
Burkina Faso inapambana na uasi ambao ulianzia nchi jirani ya Mali mwaka 2015 na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 17,000 na wanajeshi huku watu milioni mbili wakiachwa bila makaazi rasmi.
Nchi hiyo inaongozwa na serikali ya mpito iliyoingia madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Septemba mwaka 2022.