Kiongozi wa kijeshi Gabon asema hatoharakisha uchaguzi
2 Septemba 2023Katika hotuba kupitia televisheni Ijumaa (01.09.2023) Nguema amesema kuwa uongozi wa kijeshi utaendelea kuchukuwa hatua za haraka lakini kwa umakini kuepeuka chaguzi zinazorudia makosa kwa kuwarudisha viongozi wa sasa.
Soma pia:Ufaransa, Uingereza na Umoja wa Afrika walaani mapinduzi ya kijeshi Gabon
Haya yanajiri wakati muungano wa vyama vya upinzani wa Gabon, umetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhimiza viongozi waliompindua Rais Ali Bongo, kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.
Muungano wa upinzani washinikiza kuhesabiwa upya kwa kura
Msemaji wa muungano huo unaojulikana kama Alternance 2023, Alexandra Pangha, amelieleza shirika la habari la BBC kwamba wamefurahia kupinduliwa kwa Bongo, na wana matumaini kwamba viongozi wa mapinduzi watakabidhi mamlaka kwa utawala wa kiraia.