1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Kosovo yatakiwa kupunguza mivutano na Waserb

1 Juni 2023

Watu wa jamii ya serb wamekusanyika kwa siku ya nne mahali walipokabiliana na wanajeshi wa NATO kaskazini mwa Kosovo, huku shinikizo la kimataifa likiongezeka dhidi ya mamlaka ya Pristina kuitaka ipunguze mivutano.

https://p.dw.com/p/4S4jR
Kosovo | KFOR Friedensmission
Picha: Erkin Keci/AA/picture alliance

Polisi ya Kosovo imewataka watu kutoka jamii ya Albania kupuuza kampeni ya mitandao ya kijamii, iliyiwahimiza kuandamana kuelekea katika mitaa iliyo na Waserb wengi katika mji uliogawika wa Mitrovica, ili wasichochee zaidi mzozo.

Katika mji wa kaskazini wa Zvecan, waandamanaji wapatao 70 wamepiga kambi nje ya jengo la ofisi za mji, ambalo limezungushiwa senyeng'e na kulindwa na wanajeshi wa NATO waliovalia mavazi ya kupambana na vurugu.

Soma pia:Maandamano mapya ya WaSerbia yaibuka Kosovo

Wanajeshi hao wamefunga barabara kwa kutumia magari ya kivita, kwa ombi la Waserb baada ya waandamanaji waliozifunika nyuso zao kuvunja vioo vya magari mawili ya polisi na kumjeruhi afisa mmoja.