1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin: Putin yuko tayari kwa mazungumzo na Kansela Scholz

13 Oktoba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko tayari kwa mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.

https://p.dw.com/p/4ljaT
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.Picha: Kay Nietfeld/Sputnik/AP/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa Jumapili na msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, huku akibainisha kuwa hadi sasa hakuna pendekezo lolote la Ujerumani. Kauli ya Peskov ilikuwa ikijibu taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, ambaye alisema siku ya Ijumaa kuwa Putin hayuko tena katika nafasi ya kuzungumza na kansela hata kwa njia ya simu.

Soma pia: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ataka juhudi mpya za amani nchini Ukraine

Hivi majuzi, Scholz alisisitiza umuhimu wa kuzingatia uwezekano wowote wa upatikanaji amani katika vita vya Ukraine na hivyo kuzidisha uvumi kwamba Kansela huyo alitazamiwa kuzungumza kwa njia ya simu na Putin. Mara ya mwisho Scholz kuzungumza na Putin ilikuwa Disemba mwaka 2022 alipokuwa akitoa wito wa kuondolewa wanajeshi nchini Ukraine na kupendekeza suluhisho la kidiplomasia.