SiasaUrusi
Kremlin: Hakuna chochote kipya kufuatia kitisho cha Trump
23 Januari 2025Matangazo
Kremlin imesema haijaona chochote cha msingi kwenye kitisho kipya kilichotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani cha kuiwekea vikwazo vipya na ushuru ikiwa haitakubali kuvimaliza vita vyake nchini Ukraine.
Soma pia: Marais wa Urusi na Iran wasaini makubaliano ya ushirikiano
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema hata katika awamu ya kwanza, Trump mara zote aliiwekea vikwazo Urusi na kurudia tena kwamba Urusi iko tayari kwa mazungumzo yenye usawa na kuheshimiana na Marekani.
Trump alisema jana kwamba ikiwa hawatafikia makubaliano hivi karibuni hatakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuiwekea Urusi ushuru wa juu kabisa na vikwazo katika kila kitu kinachouzwa na Urusi nchini mwake pamoja na mataifa mengine washirika wa Urusi.