Kyiv yashambuliwa wakati ujumbe wa amani wa Afrika ukizuru
16 Juni 2023Ujumbe huo wa Afrika ambao unahusisha viongozi kutoka Afrika Kusini, Senegal, Comoro na Misri, ulitarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na kisha kufanya mazungumzo na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini St Petersberg kesho Jumamosi.
Shuhuda wa shirika la habari la Reuters katikati mwa mji wa Kyiv amesema aliskia milipuko miwili. Meya wa mji huo Vitali Klitschiko pia ameripoti milipuko katika wilaya ya kati ya Podil, na kuonya kwamba makombora zaidi yalikuwa yanaelekezwa mjini humo.
Mwandishi mwingine wa shirika la Reuters katika mji mkuu wa Kyiv aliona moshi mkururo wa moshi uliotokana na makombora mawili angani, lakini haikuwa wazi ikiwa makombora hayo yalifayatuliwa na Urusi au mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine.
Soma pia: Viongozi wa nchi za Afrika waanza juhudi za kusuluhisha mgogoro kati ya Urusi na Ukraine
Timu ya televisheni ya reuters imewaona viongozi wa Afrika wakiwasili mjini Kyiv katika msafara wa magari na kuingia hoteli kutumia hifadhi yake ya madhambulizi ya angani.
Ziara ya Bucha imekuwa muhimu, kwa sabau jina la mji huo limekuja kuwakilisha ukatili wa vikosi vya Moscow tangu uvamizi wake kamili wa Ukraine Februari 2022.
Ukaliaji wa kikatili wa Urusi mjini Bucha uliacha mamia ya raia wakiwa wamekufa barabarani na kwenye makaburi ya halaiki. Ujumbe wa Afrika pia unajumuisha maafisa wakuu kutoka Zambia, Uganda, Misri, na Jamhuri ya Kongo.
Ramaphosa alisema mwezi uliopita kuwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na Rais wa Urusi Vladimir Putin walikuwa wamekubali kufanya mikutano tofauti na wajumbe.
Soma pia: Afrika inahitaji kuendeleza mpango wa usafirishaji nafaka
Mapendekezo ya ujumbe
Ujumbe wa amani wa Afrika huenda ukapendekeza hatua kadhaa za kujenga kuaminiana wakati wa juhudi zake za mwanzo za upatanishi, kulinga na rasimu ya waraka ambao reuters imeona nakala yake.
Maafisa waliosaidia kuandaa mazungumzo hayo walisema viongozi hao wa Afrika hawakulenga tu kuanzisha mchakato wa amani lakini pia kutathmini jinsi Urusi, ambayo iko chini ya vikwazo vikali vya kimataifa, inaweza kulipwa kwa mauzo ya mbolea ambayo Afrika inayahitaji sana.
Pia wanatazamiwa kujadili suala linalohusiana la kuhakikisha usafirishaji wa nafaka zaidi kutoka Ukraine wakati wa vita na uwezekano wa kubadilishana wafungwa zaidi.
Ziara hiyo ya viongozi wa Afrika imejiri wakati tayari Ukraine imeanzisha operesheni kubwa ya mashambulizi kujaribu kuvijresha nyuma vikosi vya Urusi katika maeneo kadhaa.
Rais Volodymyr zelenskiy amesema mapaka sasa vikosi vyake vimefanikiwa kurejesha eneo lenye ukubwa wa kilomita 100 za mraba, na kusifu ari yao ya mapambano.
"Hatua za mashambulizi na mashambulizi ya kujibu zinaendelea nchini Ukraine - kwa hatua ambayo sitasema kwa undani. Na ninaamini kuwa hakika sote tutaihisi," alsiema Zelenskiy.
Soma pia: Ukraine yapokea ahadi zaidi za kupatiwa silaha
Mkuu wa jeshi la Ukraine Andriy Kovalev, amesema katika taarifa leo kuwa vikosi vyake vimerikodi mafanikio katika safu tatu za mstari wa mbele kusini na mashariki mwa nchi hiyo.
Mashambulizi ya usiku kucha ya Urusi yameua raia wawili na kuwajeruhi wengine wawili katika mkoa wa kusini wa Kherson, kwa mujibu wa gavana wa mkoa huo Oleksandr Produkin.
Chanzo: Mashirika