1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ujumbe wa viongozi wa Afrika wawasili Ukraine

16 Juni 2023

Kumetolewa tahadhari ya shambulizi la angani katika Mji Mkuu wa Ukraine Kyiv leo, wakati ambapo ujumbe wa viongozi wa Afrika umewasili mjini humo.

https://p.dw.com/p/4Sfq2
Viongozi wa Afrika wamanza mkakati wa kusaka amani katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine kwa kufanya mazungumzo na marais wa mataifa hayo.
Wakuu wa nchi na serikali kutoka Afrika wakiwa njiani kuelekea Ukraine wakitokea Warsaw, Poland kwa usafiri wa treni Picha: via REUTERS

Maafisa wa mji wa Kyiv wametoa tahadhari hiyo baada ya jeshi la Ukraine kusema kwamba makombora kadhaa ya Kalibr kutoka Urusi yamerushwa kutokea Bahari Nyeusi na yanaelekea Kyiv.

Haya yanafanyika wakati ambapo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa amewasili Ukraine kama sehemu ya kundi la marais wanne na wawakilishi watatu wa serikali za Afrika wanaoshughulika na juhudi za upatanishi kati ya Kyiv na Moscow.

Soma Zaidi: Ujumbe wa Afrika katika vita vya Ukraine kuanza mwezi huu

Kikosi hicho cha ngazi ya juu kinatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy leo na hapo kesho kikutane na Rais Vladimir Putin wa Urusi. Wakati huo huo, taarifa kutoka ikulu ya Kremlin zinasema Rais Putin yuko tayari kwa mazungumzo ya usuluhishi wa mzozo wa nchi yake na Ukraine.