1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Lavrov ziarani China

8 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni ya Urusi, Sergei Lavrov, amewasili nchini China kwa ziara ya kikazi, wakati mataifa hayo mawili yakiimarisha mahusiano yao huku uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiendelea.

https://p.dw.com/p/4eWWs
Waziri wa Mambo wa  Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.
Waziri wa Mambo wa Nje wa Urusi, Sergei Lavrov.Picha: Boris Grdanoski/AP Photo/picture alliance

Kupitia mtandao wa X, wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilitangaza kuwa Lavrov aliwasili mjini Beijig asubuhi ya Jumatatu (Aprili 8).

Katika ziara hiyo ya siku mbili, Lavrov alitarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Wang Yi, juu ya masuala kadhaa muhimu, ukiwemo mzozo wa Ukraine na hali kwenye eneo la Asia na Pasifiki, imesema wizara hiyo.

Soma zaidi: Moscow yaonya nchi za Magharibi kuhusu mikutano ya usalama

Mara ya mwisho kwa Lavrov kuwapo mjini Beijing, ilikuwa ni mwezi Oktoba, kwa mkutano wa jukwaa la kimataifa la mradi wa ujenzi wa miundombinu wa China, maarufu kama Belt and Road.

Panapohusika suala la Ukraine, China inajichukulia kama taifa lisiloegemea upande wowote, ingawa ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Urusi.