1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Lebanon yasema Israel lazima iondoke nchini mwake

18 Januari 2025

Rais mpya wa Lebanon Joseph Aoun amesema kwamba Israel lazima iondoke kusini mwa nchi yake kufikia tarehe ya mwisho ya Januari 26 iliyowekwa ili kutekeleza kikamilifu makubaliano ya Israel na kundi la Hezbollah.

https://p.dw.com/p/4pK60
Lebanon I Beirut | Joseph Aoun
Rais mpya wa Lebanon Joseph AounPicha: Lebanese Parliament media office/AP/picture alliance

Rais mpya wa Lebanon Joseph Aoun amesema leo kwamba Israel lazima iondoke kusini mwa nchi yake kufikia tarehe ya mwisho ya Januari 26 iliyowekwa ili kutekeleza kikamilifu makubaliano ya Israel na kundi la Hezbollah ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwaka jana.

Matamshi yake yanafuatia hotuba ya kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Hezbollah Naim Qassem ambaye aliishutumu Israel kwa ukiukaji wa usitishaji mapigano.

Soma zaidi.Rais wa Lebanon amteua jaji wa ICJ kuwa waziri mkuu 

Rais Joseph Aoun alimwambia mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyekuwa ziarani kuwa ni muhimu kwa "majeshi ya Israel kuondoka katika maeneo inayoyakalia kwa mabavu kusini mwa nchi hiyo kwa muda uliowekwa wa makubaliano yaliyofikiwa tarehe 27 Novemba mwaka uliopita.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye pia alikuwa ziarani nchini Lebanon hapo jana alisema ni lazima kuharakishwe utekelezaji wa usitishaji vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.