1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

UN yasema Maelfu wakimbia mapigano nchini Sudan

13 Januari 2025

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) limesema, maelfu ya watu wameukimbia mji wa Um Rawaba nchini Sudan baada ya kuzuka mapigano wiki iliyopita kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

https://p.dw.com/p/4p6ae
Sudan | Madhara ya mashambulizi kati ya jeshi na RSF
Mkaazi wa Sudan akiangalia madhara kufuatia mashambulizi yaliofanyika katika makaazi yake.Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Kwa mujibu wa Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, watu kutoka kwenye kaya 1,000 hadi kaya 3,000 walilazimika kuukimbia mji wa Um Rawaba ulio katika jimbo la Kordofan la Kaskazini kusini mwa Sudan katika muda wa siku tano.

Soma pia:UN: Maefu ya Wasudan wayakimbia mapigano huko Um Rawaba

IOM imesema zaidi ya watu laki mbili na tano wamekimbia makazi yao kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi wa usalama wakati ambapo mapigano yanaendelea katika eneo la Kordofan.

Nchini Sudan, watu milioni 11.5 wamegeuka kuwa wakimbizi wa ndani wakiwemo watu 2.7 waliokimbia makazi yao katika migogoro ya hapo awali. Umoja wa Mataifa umeutaja mzozo wa wakimbizi wa Sudan kuwa ni mkubwa zaidi duniani.