1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Maafisa watatu Uganda washtakiwa kwa mauaji bila kukusudia

19 Oktoba 2024

Mahakama moja ya Uganda imewafungulia mashtaka maafisa watatu wa zamani wa Mamlaka ya Jiji la Kampala kwa mauaji bila kukusudia kuhusiana na maporomoko katika eneo moja la kutupa taka, yaliosababisha vifo vya watu 35.

https://p.dw.com/p/4lz5p
Majaji wa mahakama ya kikatiba nchini Uganda wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushoga mnamo Desemba 18, 2023.
Majaji wa mahakama ya kikatiba nchini UgandaPicha: Hajarah Nalwadda/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa polisi nchini Uganda Kituuma Rusoke, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba maafisa hao watatu walishitakiwa kwa makosa 57.

Washitakiwa hao watawekwa kizuizini hadi Novemba 4 ambapo wataruhusiwa kutuma maombi ya dhamana.

Soma pia:Watu wasiopungua 18 wauawa katika maporomoko ya taka Uganda

Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, aliwafuta kazi maafisa hao watatu mwezi Septemba.

Mnamo mwezi Agosti, rais huyo pia aliagiza malipo kwa familia za waathiriwa ya dola 1,300 kwa kilakifo na dola 270 kwa kila aliyejuruhiwa.