1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano nchini Georgia yaendelea kwa siku ya saba

5 Desemba 2024

Kwa usiku wa saba mfululizo maelfu ya raia wa Georgia ambao ni wafuasi wa Umoja wa Ulaya wanaandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Tbilisi wakiipinga serikali ya kitaifa ya kihafidhina.

https://p.dw.com/p/4nmDo
Georgien ITbilisi |
Kwa usiku wa saba mfululizo maelfu ya raia wa Georgia ambao ni wafuasi wa Umoja wa Ulaya wanaandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo TbilisiPicha: Zurab Tsertsvadze/AP Photo/picture alliance

Kwa usiku wa saba mfululizo maelfu ya raia wa Georgia ambao ni wafuasi wa Umoja wa Ulaya wanaandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Tbilisi wakiipinga serikali ya kitaifa ya kihafidhina. Wakati maandamano hayo yakiendelea nchini Georgia nchi jirani ya Ukraine imemuwekea vikwazo Waziri Mkuu wa Georgia Bidzina Ivanishvili, anayeonekana na wengi kama kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Waandamanaji nchini Georgia waliizingira mitaa na kuzifunga barabara katika mji mkuu wa Georgia wakitaka kuendelezwa kwa sera zinazounga mkono Umoja wa Ulaya katika nchi hiyo ambayo zamani ilikuwa Jamhuri ya Kisovieti.

Soma zaidi. Maandamano yaendelea Georgia kwa siku ya saba mfululizo

Haya yote yanafanyika baada ya uamuzi wa chama tawala kinachoiunga mkono Urusi cha Georgian Dream kukamwisha mchakato wa nchi hiyo kujiunga katika Umoja wa Ulaya wiki kadhaa zilizopita.

Georgia
Picha za waandamanaji nchini GeorgiaPicha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Kila ikifika majira ya jioni katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tbilisi vikosi vya polisi na vikosi vya kijeshi vimekuwa vikikusanyika katika viunga vya mji huo kukabiliana na waandamanaji ingawa hakuna hatua kali zilizochukuliwa kwa waandamanaji wanaojitokeza.

Hata hivyo, duru za ndani za nchi hiyo zinasema wanasiasa wengi wa upinzani wamekamatwa siku ya Jumatano.

Soma zaidi. Polisi nchini Georgia yawakamata waandamanaji 107 katika mji mkuu Tbilisi

Kupitia mtandao wa X, msemaji wa mkuu mpya wa sera ya nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, alitoa ripoti iliyoelezea kuwepo kwa vitendo vya kukamatwa kiholela, vurugu, na unyanyasaji wa waandamanaji huko akizitolea mwito pande zote kutojihusisha na vurugu.

Hali hiyo inayoendelea nchini Georgia imesababisha kujiuzulu kwa baadhi ya wanadiplomasia na watumishi wengine wa umma, ikiwa ni pamoja na afisa mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, hayo ni kulingana na shirika la habari la Georgia Interpressnews.

Ukraine yaweka vikwazo kwa waziri mkuu wa Georgia

Katika hatua nyingine, Rais wa Ukraine Volodmir Zelensky amesema kupitia mtandao wa telegram kwamba serikali ya Georgia ni kama inajikabidhi kwa Urusi.

Rais wa Ukraine Vladymir Zelensky
Rais wa Ukraine Vladymir ZelenskyPicha: IMAGO/ZUMA Press Wire

Zelenskyy ''Serikali ya sasa ya Georgia inaisukuma nchi kuelekea kwenye utegemezi wa wazi kwa Urusi. Ni aibu wanachofanya dhidi ya watu wao. Na wakati Moscow inaisifu serikali hii ya Georgia, inaonyesha wazi ni nani wanafanya kazi huko Tbilisi na nani wanatawanya maandamano, kwa hakika si kwa ajili ya Georgia."

Kufuatia hatua hiyo, Ukraine imemuwekea vikwazo Waziri Mkuu wa Georgia na bilionea Bidzina Ivanishvili, anayeonekana na wengi kama kiongozi mkuu wa nchi hiyo.