SiasaUfaransa
Maandamano ya wakulima yasambaa Ulaya kabla ya mkutano wa EU
31 Januari 2024Matangazo
Nchini Ubelgiji, wakulima walifunga barabara zinazoelekea bandari ya shehena ya Zeebrugge ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini humo.
Walisema wanalenga kuzruia barabara za kuingia katika bandari hiyo kwa saa 36 kwa sababu wanasema inapokea msaada wa kiuchumi badala ya wakulima.
Maandamano hayo yameongeza kasi kabla ya kufanyika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya kesho Alhamisi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema atalijadili suala hilo na rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen na viongozi wa serikali za umoja huo.
Maandamano hayo yanafuatia mengine sawa na hayo yaliyofanywa na wakulima karibu kote barani Ulaya ikiwemo nchini Ujerumani, Poland na Romania.