Wakulima wa Ujerumani waandamana nje ya maonyesho ya kilimo
20 Januari 2024Matangazo
Wawakilishi wa muungano unaojiita "Tumechoshwa" waliwasilisha barua ya malalamiko yao kwa waziri wa kilimo Cem Özdemir.
Wakulima hao wanapinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kwenye vyombo vya moto vinavyotumika katika kilimo.
Maandamano hayo yalijumuisha wakulima wazee na vijana pamoja na makundi mengine kama vile wafugaji nyuki. Wamehimiza kuwepo kwa sekta ya kilimo iliyoboreshwa, urasimu mdogo na kuimarishwa kwa demokrasia.
Maandamano hayo yalitarajiwa kupita katikati ya mji mkuu Berlin na kukamilika mbele ya ofisi ya Kansela Olaf Scholz.