1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yahanikiza siku ya kimataifa ya wanawake

8 Machi 2023

Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake yamefanyika leo kote duniani kutetea haki ambazo zinazidi kushambuliwa.

https://p.dw.com/p/4OPHV
Serbien Nis | Geschlechtergerechtigkeit
Picha: Jelena Djukic Pejic/DW

Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake yamefanyika leo kote duniani kutetea haki ambazo zinazidi kushambuliwa. Yamefanyika baada ya mwaka ambao wasichana nchini Afghanistan walipigwa marufuku kupata elimu, maandamano makubwa ya wanawake yalizuka nchini Iran na uamuzi wa kistoria wa uavyaji mimba nchini Marekani ulibatilishwa.

Maandamano yalifanywa Paris, Berlin, Beirut, Jakarta, Singapore na kwingineko. Mjini Manila, Ufilipino, wanaharakati waliandamana kudai haki sawa na mishahara bora kabla ya polisi kutawanywa na polisi. Mjini Melbourne, waandamanaji walidai malipo sawa na usalama bora kwa wanawake. Katika ujumbe wake wa siku hii ya kimataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres alionya kuwa haki za wanawake zinatoweka mbele ya macho yetu, akisema suala la usawa wa jinsia litachukua karne nyingine tatu ili kutimizwa.