Marekani watupwa nje Kombe la Dunia na Sweden
7 Agosti 2023Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia la Wanawake Marekani wametupwa nje ya michuano hiyo.
Michuano ya Kombe la Duniani kwa Wanawake bado inaendelea nchini Australia na New Zealand na ulimwengu unaendelea kushuhudia matokeo ya kushangaza mara baada ya mabingwa watetezi Marekani kutolewa nje ya mashindano hayo katika hatua ya 16 bora na Sweden kupitia mikwaju ya penalti huko mjini Melbourne.
Soma zaidi:Nigeria yaaga Kombe la Dunia la Wanawake
Marekani walitawala karibu dakika zote 120 za mchezo huo lakini mechi iliishia kumalizika bila bao na kupelekea penalti kuamua matokeo ambapo Sweden walifunga penalti 5 dhidi ya 4 za Marekani.
Nyota wa Marekani Megan Rapinoe aliyekuwa anacheza kombe lake la mwishio alikosa penati, pamoja na wachezaji wengine watatu wa Marekani na kuipa nafasi Sweden ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Soma zaidi:Kenya: Waathirika wa mashambulizi ya ubalozi wa Marekani bado kufidiwa
Marekani inayoongoza kwa viwango vya ubora duniani vya FIFA kwa upande wa wanawake inaungana na mataifa mengine makubwa kama Ujerumani na Italia ambayo yametupwa nje ya mashindano hayo.
Sweden sasa itacheza robo fainali na Japan ambayo imeitoa Norway siku ya Ijumaa.